Round ya nne ya michuano ya UEFA Champions League hatua ya makundi iliendelea usiku wa November nane kwa michezo nane kuchezwa barani Ulaya, game ya Tottenham Hotspurs dhidi ya Real Madrid ni miongoni mwa game zilizochezwa usiku wa November 1.

Real Madrid walilazimika kutoka Hispania hadi London England kucheza mchezo wao wa marudiano wa hatua ya makundi ya UEFA Champions League dhidi ya Tottenham , baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1.

Mchezo wa marudiano uliyochezwa katika uwanja wa Wembley, Tottenham Hotspurs wamefanikiwa kuifunga Real Madrid kwa jumla ya magoli 3-1, magoli ya Tottenham yakifungwa na Dele Alli aliyefunga magoli mawili dakika ya 27 na 56, goli la tatu likafungwa na Christian Eriksen dakika ya 65, wakati goli pekee la Real Madrid lilifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 80.

Ushindi huo sasa unavunja rekodi ya Real Madrid iliyodumu kwa kipindi cha miaka mitano toka mwaka 2012, kwani kipigo hicho kinaifanya Real Madrid kufungwa kwa mara ya kwanza katika mchezo wa hatua ya makundi toka 2012 lakini kipigo hicho kimetoa nafasi kwa timu za Apoel na Borussia Dortmund kuwa na nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora.

Msimamo wa Kundi H ulivyo kwa sasa baada ya matokeo ya game za November 1 2017.