Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Billy Mwakatage (wa nne kulia ), akipokea msaada wa simu kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Halotel Bw. Trieu Binh (wa tatu kushoto) katika makabidhiano yaliyofanyika Makao Makuu ya Halotel jijini Dar es Salaam leo hii.

Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Bw. Trieu Binh (katikati) akizungumza na Ugeni kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania ukiwakilishwa na Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy Mwakatage (kulia) ) katika makabidhiano ya msaada wa simu yaliyofanyika Makao Makuu ya Halotel jijini Dar es Salaam leo hii

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy Mwakatage (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Halotel (hayupo pichani) katika makabidhiano ya msaada wa simu yaliyofanyika Makao Makuu ya Halotel jijini Dar es Salaam leo

Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Bw. Trieu Binh akiteta jambo na Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Billy Mwakatage, walipokutana ofisi za Makao Makuu ya Halotel Jijini Dar es Salaam katika makabidhiano ya msaada wa simu leo hii tarehe 02/11/2017

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel Bw. Mhina Semwenda (kushoto) akielezea jambo kwa Kamishna na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawako pichani), walipokutana ofisi za Makao Makuu ya Halotel Jijini Dar es Salaam katika makabidhiano ya msaada wa simu leo hii tarehe 02/11/2017

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Billy Mwakatage akimpa mkono wa shukurani Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Bw. Trieu Binh kwa msaada walioutoa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji hii

Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji

……………

Kampuni ya simu za mikononi Halotel imetoa msaada wa simu kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano ya namba ya dharura 114, katika makabidhiano yaliyofanyika mchana wa leo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo ambayo ilifanyika Makao Makuu ya Halotel Naibu Mkurugenzi Bw. Trieu Binh, alisema wametoa msaada huo ili kusaidia jamii kuwapata haraka Jeshi la Zimaoto na Uokoaji kwa kutumia matandao wa halotel.

Naye Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy Mwakatage, ambaye amepokea msaada huo, amesema ‘‘msaada huu utakuwa chachu kwa Jeshi na utarahisisha mawasiliano kati yetu na jamii wakati yanapotokea majanga’’

Kamishna Mwakatage ameahidi kuzigawa simu hizo kwenye vituo vya Zimamoto na Uokoaji hapa nchini ili kuongeza wigo mapana wa mawasiliano haswa kwa wateja wa halotel kwani mwanzo huduma hiyo ilikuwa haipatikani kwa kupiga 114.

Sanjari na kupokea msaada huo, Kamishna Mwakatage aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada walioutoa na kuwaomba waendelee kushirikiana na Jeshi hilo katika nyanja nyingine mbalimbali ili kuboresha huduma kwa jamii