Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Mimi Mars amesema kwa sasa anatamani Jux na Vanessa Mdee warudiane.

Muimbaji huyo ambaye ni ndugu wa damu na Vanessa, katika mahojiano na kipindi cha Clouds E pia alielezea kuchukizwa na taarifa zinazodai kuwa anatoka kimapenzi na Jux baada ya kuachana na Vanessa.

“Kwanza nilikasirika kwa sababu ni kukoseana heshima, ina maanisha watu wananionaje kwanza, mnanichukuliaje kwamba mimi naweza nikafanya tendo na mtu wa dada yangu haileti maana kabisa, niliipuuzia ndio maana sijaizungumzia” amesema Mimi Mars.

“Mungu akijalia kweli I wish warudiane maana yake walikuwa poa, (Jux) ni mtu mcheshi, ana upendo, mtu mkarimu na ni mtu anayempenda Vanessa Mdee” ameongeza.

Alipoulizwa anauchukuliaje ukaribu wa sasa kati ya Jux na Vanessa, alijibu; “kama mimi naona ni marafiki kama walivyotuambia ambao wanaendelea kuwa na uhusiano mzuri, maana tumejiwekea watu wakiachana lazima wawe maadui siyo lazima iwe hivyo, kwa hiyo wao wanatuonyesha njia tofauti”