Miezi inahesabiki kuelekeza mwezi June 2018 michuano ya Kombe la Dunia 2018 itakapoanza kutimua vumbi kule nchini Urusi kwa mataifa 32 kuanza kupimana nguvu kisoka, hadi kufikia jana November 11 2017 ni mataifa 25 ndio yamefuzu.

Bara la Afrika ambao hutoa mataifa matano katika kila michuano ya Kombe la Dunia, litawakilishwa na nchi za Tunisia, Nigeria, Morocco, Senegal na Misri kwani hizo ndio timu zilizokuwa zimefuzu lakini michuano ya 2018 ndio kwa mara ya kwanza tutaona mataifa manne ya kiarabu kwa pamoja yakishiriki michuano hiyo (Misri, Tunisia, Morocco na Saudi Arabia.

Kuna michezo saba ya mwisho ya Play off ambayo ndio itaamua timu gani saba pamoja na mwenyeji Urusi zitaungana na zile 25 kucheza Kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

LIST YA MATAIFA 25 YALIOFUZU KUCHEZA KOMBE LA DUNIA 2018

1- Nigeria 2- Morocco 3- Misri 4- Tunisia 5- Senegal 6- South Korea 7– Saudi Arabia 8– Japan 9– Iran 10– Panama 11– Costa Rica 12– Mexico 13– Uruguay 14– Colombia 15– Brazil 16– Argentina 17– Hispania 18– Serbia 19– Ureno 20– Poland 21– Iceland 22– Ujerumani 23– Ufaransa 24– England 25– Ubelgiji 26– Urusi