Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Tulia Ackson akitoa majibu ya miongozo mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa kikao cha sita cha Bunge hilo leo Mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk Ndugulile akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dk. Harrison Mwakyembe akisoma kauli yake kuhusu fursa kwa wasichana kujipima uwezo katika riadha ili waweze kuiwakilisha nchi katika mashindano yajayo ya kimataifa ya Jumuiya ya Madola, Olimpiki, All-African games na mengineyo leo Bungeni mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso wakati wa Mkutano wa tisa kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe.Dk. Mary Mwanjelwa wakati wa Mkutano wa tisa kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Dodoma.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.