Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib Ayoub Mahmoud amepiga marufuku usafiri wa Boda boda kutumika Zanzibar kutokana na vitendo vya wizi na ajali za kila mara.

Ikiwa ni Siku ya mwisho kwenye Ziara yake ya siku 10 kufika mwisho,imemalizika kwa kishindo huku Wananchi wakionekana kufurahishwa na kumuomba awe anafanya hivyo kila anapopata nafasi.

Katika kuhitimisha Ziara hii amepokea kero ya Muziku mkubwa unaopigwa Ukumbi wa Bwawani ambapo unamilikiwa na Mfanyabiashara Hussain Makungu ambaye pia ni Mwakilishi jimbo la Malindi kwa kuonesha jeuri yabkupiga mziki unaotoa sauti kwenye jamii ya watu.

Muheshimiwa Ayoub baada ya kupokea kero hiyo ameamuru kutokufanyika shuguli zozote zile za Muziki na Bar katika Hotel ya Bwawani.

“Naamuru kumbi hizo zifingwe kutokana na wamiliki kuzarau uongozi wa Serikali hivyo tunafungua hadi pale Serikali itakapo amua kuwafungulia tena” Amese.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ameifungia nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Lulu Guest House iliyopo Shehia ya Mwembetanga kwa kuendesha biashara hiyo kinyume na taratibu badala ya kulaza wageni tu.

Kero zingine zilizotajwa ni za maji,Barabara ,choo cha Umma,mitaro na ujenzi holela ambapo vyote vimechukuliwa na wahusika wa Manispaa wametakiwa kutatua changamoto hizo.

Hata hivyo Wananchi wengi wamempongeza Rc. Ayoub kwa ziara yake ya siku kumi kwa kulisikiliza kero za wananchi jambo ambalo halijawahi tokea na viongozi wengine waige mfano wake.

Ziara hiyo imehitimishwa katika Viwanja vya Malindi ambapo alianzia katika Kiwanja cha Mpira cha Dimani.