Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisalimiana na Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI) wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua mkutano wa kumi na moja uliowakutanisha wanasayansi wa utafiti wa wanyamapori wapatao 300 kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana ujuzi katika mkutano huo unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kumi na moja uliowakutanisha wanasayansi wa utafiti wa wanyamapori wapatao 300 kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI) kwa ajili ya kubadilisha ujuzi wa tafiti unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC wa jijini Arush

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikabidhiwa cheti na Mwenyekiti wa Bodi ya TAWIRI, Prof. Apolinaria Pereka cha kutambua mchango uliofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kufanikisha mkutano wa kumi na moja wa uliowakutanisha wanasayansi wa utafiti wa wanyamapori wapatao 300 kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana ujuzi unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC wa jijini Arusha

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza katika mkutano wa kumi na moja uliowakutanisha wanasayansi wa utafiti wa wanyamapori wapatao 300 kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana ujuzi ulioandaliwa na TAWIRI unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC wa jijini Arusha

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Dkt. Simon Mduma akizungumza katika mkutano wa kumi na moja uliowakutanisha wanasayansi wa utafiti wa wanyamapori wapatao 300 kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana ujuzi unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC wa jijini Arusha

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya kufungua mkutano wa kumi na moja uliowakutanisha wanasayansi wa utafiti wa wanyamapori wapatao 300 kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI) kwa ajili ya kubadilisha ujuzi wa tafiti unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC wa jijini Arusha

Picha na Lusungu Helela-MNRT

……………..

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa mmea hatari uitwao gugu karoti hauoti katika maeneo ya hifadhi kwa kuwa una madhara makubwa kwenye malisho ya wanyamapori .

Amesema mmea huo ukiota ndani ya maeneo ya hifadhi umekuwa ukizuia uoto asili kuota na hivyo kupelekea kutoweka kwa malisho ya wanyamapori.

Amesema mmea huo ulibainika miaka tisa iliyopita na umekuwaa ukisambaa katika maeneo ya nje ya hifadhi na athari zake zimekuwa zikionekana wazi wazi.

Amesema baada ya matokeo ya utafiti kuhusiana na mmea huo, Serikali imeamua kuiongezea bajeti Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) ili iweze kufanya tafiti zaidi kuhusiana na mmea huo.

‘’Serikali kupitia Wizara yangu tumejipanga kuhakikisha kuwa mmea huo unatokomezwa kabisa.’’ Alisisitiza Hasunga.

Alibainisha hayo leo mjini Arusha katika Mkutano wa utafiti wa kisayansi uliowakutanisha Wanasayansi 300 waliofanya tafiti mbalimbali katika hifadhi za wanyamapori na mazingira kwa ujumla wa kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Mkutano huo umeanza leo na utafanyika kwa muda wa siku tatu ambapo wanasayansi watafiti mbalimbali wataziwasilisha na kuzijadili tafiti zao zipatazo 167 katika maeneo hayo.

Aidha, Naibu Waziri Hasunga amesema mkutano huo utatoa nafasi ya kubadilishana uzoefu, mawazo na pia ni fursa ya kutangaza vivutio vya utalii tulivyonavyo kwa wanasayansi hao.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TAWIRI, Prof. Aporinalia Pereka amesema kwa upande wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) nao tayari wameanza kufanyia utafiti mmea huo ili usiweze kusambaa zaidi kwa kuwa una madhara kwa wanyamapori na kwa binadamu pia.

Amesema kwa upande wa binadamu mmea huo umekuwa na madhara katika ngozi na upande wa wanyamapori umekuwa ukiathiri uoto asili na hivyo kupelekea malisho ya wanyamapori kutoweka.

Wakati huo huo, Mwenyekiti huyo wa Bodi,Prof. Pereka ameiomba serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iendelee kutenga bajeti ya kutosha ili Taasisi hiyo iweze kufanya tafiti nyingi zaidi katika maeneo mengi ya nchi tofauti na sasa inavyofanya.