Mgeni rasmi, Naibu Spika wa Bunge la Kenya, Mheshimiwa kemboi Cheboi (kushoto) akisalimiana na wachezaji wa mpira wa wavu wa timu ya Tanzania, kabla ya kuanza kwa mashindano ya mchezo huo kati ya Timu ya Tanzania na Uganda uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo ni ya Nane ya Mabunge ya nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki yalioanza tarehe 1 Desemba na kumalizika tarehe 11 Desemba, 2017

Mchezaji wa timu ya mpira wa wavu wa Tanzania akiifungia timu yake goli katika mpambano kati ya Tanzania na Uganda, mchezo uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Tanzania iliibuka na ushindi wa seti 3 – 0 dhidi ya Uganda

Mashabiki wa timu ya Tanzania wakishangilia ushindi dhidi ya timu ya Uganda baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa mpira wa wavu uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Tanzania wakijiandaa kwa mchezo wa mpira wa wavu dhidi ya timu ya Uganda uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wa mpira wa wavu uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

PICHA NA OFISI YA BUNGE