MKUU WA JESHI LA POLISI IGP SIMON SIRRO, AKIZUNGUMZA NA ASKARI WA VIKOSI VYA MJINI MAGHARIBI, KUSINI UNGUJA NA KASKAZINI UNGUJA JANA ALIPOKWENDA KUFANYA MAZUNGUMZO YA KIKAZI NA MAOFISA NA ASKARI VISIWANI UNGUJA. IGP SIRRO ALIWATAKA ASKARI VISIWANI HUMO KUHESHIMU WANANCHI WAKIWA KWENYE KAZI ZAO ILI KUENDELEA KULETA HESHIMA YA JESHI LA POLISI