Waziri wa mambo ya ndani ya nchi  na Mbunge wa jimbo la Iramba Dkt.  Mwigulu Nchemba akiongea na vijana waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda waliyopo stand kuu ya mabasi iramba kuhusu usalama wao waendeshapo pikipiki

……………………………………………………………………………..
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi  na Mbunge wa jimbo la Iramba Dkt. Mwigulu Nchemba leo amewatembelea wafanyabiashara ndogondogo katika soko kuu la wilaya ya Iramba, Madereva wa pikipiki na madereva wa daladala na makodakta waliopo stendi kuu ya mabasi Kiomboi ili kusikiliza changomoto wanazokutana nazo katika utendaji wao wa kazi za kila siku na kuwasilisha katika balaza la madiwani.

Kwa upande wa madereva wa bodaboda Dkt. Mwigulu amewashauri waendeshe bodaboda zao kwa usalama na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na kukamatwa mara kwa mara na askari polisi pale wanapofanya  makosa.

Wafanyabiashara ndogondogo wa soko kuu la mji wa Kiomboi wamemuomba mbunge wao kuwasaidia kupunguza kodi nyingi ambazo wanakutana nazo wakati wanafanya biashara katika soko hilo, ombi lao limepokelewa na Dkt. Mwigulu na ameahidi kukaa nao ili kuona njia nzuri za kutatua changamoto zao.

Baraza la madiwani linatarajia kukutana  mchana  leo ambapo changamoto mbalimbali alizozipokea  ataziwakilisha kupata utatuzi katika kikao hicho.