Mwanasheria Mkuu wa nchi ya Kenya Profesa Githu Muigai amejiuzulu cheo hicho mchana wa leo baada ya kutumikia nafsi hiyo kwa muda wa miaka sita na nusu.
Taarifa hiyo imethibitishwa na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta na kudai amepokea barua ya kujiuzulu Prof. Githu kwa masikitiko makubwa, hata hivyo Uhuru ametangaza nafasi hiyo kwa sasa itachukuliwa na Jaji Paul Kihara Kariuki.
Kwa upande mwingine, Rais Uhuru Kenyatta amemteua Abdikadir Mohammed kuwa Balozi wa South Korea.