PART 32: “MY AMERICAN EXPERIENCE” pichani ni unapotaka kusoma USA unapeleka vyeti vyako vyote at the “World Education Services” wao wana Evaluate level yako kielimu kwa USA System unaweza ukawa sawa na umemaliza High School au Mwaka wa Pili College in my Case my Evaluation was my Education level in USA was Equivalent to Holding one Degree kabla sijaanza Westchester College so now nkafanya Mtihani wa kuingia Lehman College mwanzoni nilitaka kusoma Sheria lakini pesa yake ikawa ndefu mno na mpaka kufikia nilipokua Shule ilikua imenila almost nusu ya pesa zangu nilizikua nimerundika Benki nikaamua nataka kusoma Political Science..Wabongo wengi wakawa wananicheka sana kua kwa nini ninapoteza pesa na Shule badala ya ku invest bongo kama wao binafsi nilikua nawacheka sana moyoni cause nilijua hawajui maana ya Elimu niliwaambia guys msichoelewa ni kwamba back in Bongo nilishajifunza hakuna mtu aliyesoma ana njaa ila wasiosoma tu na nikawakumbusha umuhimu wa kujua the truth kwamba sisi ambao tupo Majuu bila kupelekwa na Serikali au Kazi za Kimataifa ni Wakimbizi wa Uchumi infact ni LIFE FAILURES tumeshindwa Maisha Bongo that is a simple truth Mungu katupa a second chance ya kufika Majuu cha msingi kwanza tunatakiwa tusome hahaha niliishia kujiongezea Chuki na wabongo kuwa “ANJIFANYA MJUAJI SANA” …mtihani Lehman nilishinda sasa ikaja kuonyesha makaratasi ya kuishi USA kwa bahati sana msimamizi wa hiyo section alikua Mhaiti Mmarekani nikamuomba tuongee pembeni nikaamua kujilipua nikampa ukweli kua sina makaratasi ila ninazo pesa ninataka Elimu mimi ni Muafrika Masikini lakini napenda Elimu nilikua naongea mfululizo ili asipate nafasi ya kufikiri hiyo ni moja ya mbinu za mtaani ukitaka kumchanganya mteja asiyeelewa..Mhaiti akaniangalia kwa huruma akaniambia atanipa nafasi ila nimuhakikishie kua nitasoma sitamuangusha in the end akaniingiza kama Mmarekani kwa kutumia Social Security Card Number na Licence Number Sheria inasema Raia wa US anahitaji vitu hivyo 2 tu sijasahau furaha ya kukubaliwa kusoma tena na this time Political Science kwa wabongo nikaendelea kuwa gumzo lao infact walikua wananijadili kama nina akili sawa sawa… WAZO LA KUOA! ..ITAENDELEA