Msanii wa bongo fleva Bonge La Nyau amefunguka na kudai kimya chake cha muda mrefu katika muziki ni kutokana na yeye kubahatika kupata mtoto wa kike ambae ampa jina la Malaika.

Bonge la Nyau amesema mama wa mtoto huyo sio mtu maarufu kama wanavyotarajia kusikia.
“Hapa kati nilikuwa na mambo ya kifamilia nilipata mtoto kwa hiyo kuna malezi yanahitajika ili mtoto akue afike hata mwaka kidogo. Kwa hiyo kuna vitu fulani hivi lakini nimerudi”, amesema Bonge la Nyau.