Rais John Magufuli ametoa pole kwa familia, ndugu, wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) na wote walioguswa na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji kilichotokea Ijumaa wiki hii na ameagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hilo.