Rapa wa kike wa bongo Chemical ‘mwana wa Lubao’ amefunguka na kudai wanawake wa aina yake wako vizuri sana katika masuala ya kimapenzi japokuwa watu hawafahamu hilo.

Chemicala amebainisha hayo baada ya kuenea picha zake katika mitandao ya kijamii zikimuonesha akiwa na mwanaume wakinyonyana ndimi na mtayarishaji wake muziki anayefahamika kwa jina la Maxmaizer.
“Watu kama sisi ni ‘very romantic’ basi tu huwa hawafahamu. Na sisi hatutakagi kuwaonjesha kwa sababu tunaogopa wanang’ang’ania. Ile sio kiki ‘but’ zile zilipigwa kipindi tupo ‘location’ kwa ajili ya kutumiwa katika video na nyingine zikatumika kama picha tu za kawaida”, amesema Chemical.