Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akivishwa vazi la kimila la Kimasai tayari kwa Maadhimisho ya Siku ya Ukeketetaji yaliyofanyika katika Kijiji cha Elerai Kata ya Kiberashi Wilaya Kilindi Mkoani Tanga.

Laigwenani Mkuu wa Kabila la Kimasai Mzee Simon Mchamya akitoa maoni yake kwa Mgeni rasmi hayuko pichani kuhusu masuala ya ukeketeji katika jamii ya Wamasai wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukeketetaji yaliyofanyika katika Kijiji cha Elerai Kata ya Kiberashi Wilaya Kilindi Mkoani Tanga. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akipewa ufafanuzi wa shughuli zinazofanywa na shirika la kimataifa la AMREF na Meneja wa shirika hilo Wilayani Kilindi Dkt. Jane Sempaluo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukeketetaji yaliyofanyika katika Kijiji cha Elerai Kata ya Kiberashi Wilaya Kilindi Mkoani Tanga.

Wanawake wa Jamii ya Kimasai wakiigiza namna binti wa Jamii ya Kimasai anavyopelekwa ndani kwa ngariba kwa ajili ya kufanya tohara Jamii hiyo kwasasa inaachana na mira hiyo potofu na kuendelea na tohara mbadala baada ya kupatiwa elimu kuhusu madhara ya tohara na shirika AMREF.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wamasai waliopatiwa vyeti baada ya kushiriki na kukubali kuachana na mira ya tohara swakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukeketetaji yaliyofanyika katika Kijiji cha Elerai Kata ya Kiberashi Wilaya Kilindi Mkoani Tanga.

Ngariba wa Jamii ya Wamasai wameteketeza vifaa vyote vyote vya kufanyia tohara baada ya Shirika la Kimataifa la AMREF kutoa elimu ya tohara mbadala inayowawezesha Wamasai kuendelea na mira zao bila kufanya tohara kama ilivyokuwa desturi yao.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wadau wote wa Maendeleo wanaojihusisha na masuala ya kupambana na ukeketaji kuendelea na juhudi hizo kwa maslahi mapana ya Afya ya mama na mtoto.

Amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku moja ya kupinga ukeketaji yaliyofanyika Wilayani Kilindi katika kijiji cha Elerai kata ya kiberashi kijiji ambacho asimilimia kubwa ya wakazi wake ni Jamii ya Wamasai.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la AMREF Tanzania Dkt. Frolence Temu akitoa hotuba yake kwa Naibu Waziri wa Afya amesema Maadhimisho ya Siku moja kuhusu Siku ya Kimataifa ya Ukeketeji Duniani yamefanyika kijini hapo kwa kuwa shirika lake limechagua kufanya maadhimisho kwa Jamii ya mahitaji tofauti na maadhimisho yafanyikayo maeneo ya mijini.

Maadhimisho haya ufanyika kila tarehe 6 Mwezi wa pili lakini imeadhimishwa leo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na AMREF Tanzania.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustini Ndugulile amesema kuwa Kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia na Afya Tanzania ya mwaka 2015/16 inaonyesha kuwa mwanamke 1 kati ya 10 nchini amekeketwa.

Ametaja mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukeketejji kuwa ni mikoa inayoongoza kwa ukeketaji ni Manyara (58%), Dodoma (47%),Arusha (41% ), Mara ( 32%) na Singida (31%).

Waziri amesema lengo la maadhimisho haya ni kulindawanawake na watoto wa kike dhidi ya mila na desturi zenye madhara na kuzorotesha maendeleo yao wakati huohuo akiwataka AMREF na mashirika mengine yenye mtazamo sawa wa kupinga ukeketaji Tanzania kwa kutetea haki na maslahi bora ya watoto hapa nchini.

Aidha kupitia maadhimisho haya tutaweza kujipima ni kwa namna gani tumeweza kukabiliana na ukeketaji na changamoto zilizojitokeza katika mapambano haya ili kubuni mikakati mipya ya kutokomeza ukeketaji nchini.

Waziri Ndugulile ameyataja madhara yatokanayo na ukeketeji kuwa ni pamoja na kupoteza damu nyingi na kusababisha vifo, maambukizi ya VVU/UKIMWI na kusababisha matatizo wakati wa kujifungua.

Ameongeza kuwa Watoto wakati wa kukeketwa hawawezi kuhudhuria vipindi mashuleni kwa muda mrefu na hivyo kuzorotesha maendeleo yao kielimu na kuongeza kuwa Serikali inapinga, inalaani na kukemea tabia ya kuendelezwa kwa vitendo hivi vya ukatili unaomdhalilisha mtoto wa kike na mwanamke kwani unamsababishia madhara makubwa kiafya, kielimu, kisaikolojia na kimaendeleo.