MUUZA nyago aliyetamba kwenye video ya msanii wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ anakiri kwamba, mwanaume atakayemuoa anatakiwa ajipange na akubaliane na staili ya maisha yake.

Shupa aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, amezoea maisha ya kuhangaika ya kujitafutie mwenyewe, sasa kama mwanamme atataka ajibweteke hatayaweza.

“Naona kabisa mwanaume atakayetaka kunioa, kama atanizungua kwa sababu mimi ni mtafutaji, ajipange maana atafungasha virago mwenyewe,” alisema Shupa.