STAA wa kitambo kwenye Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ anaamini kuwa dharau na kejeli alizopitia kwenye tasnia hiyo ndizo zilizomfanya leo kusimama na kujulikana kila upande kwa sababu alijiamini.

Odama aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kama angekubali dharau za kwamba hawezi, basi leo hii angekata tamaa, lakini matokeo yake, zimemfanya kuwa bora zaidi na kuwakamata mashabiki lukuki.
“Mtu akikudharau na wewe ukakubali, basi atakudidimiza siku zote na huwezi kupiga hatua, lakini ukijikubali, utafika popote pale kama ilivyo mimi leo hii,” alisema Odama ambaye kwa sasa anatamba na sinema yake ya Kiongozi.