SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewataka Waratibu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) na Watendaji mbalimbali wa kuhakikisha wanasaidia walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kutumia fedha wanazozipata kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo ili hatimaye waweze kuondokana na umasikini.

Kauli hiyo jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Rehema Nchimbi wakati akiongea na Watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwenye semina ya TASAF iliyowashirikisha Maafisa Tarafa, Maafisa Ugani, Watendaji wa Vijiji na Kata , Wenyeviti wa Vijiji na Waratibu Elimu.

Alisema lengo la kuwapa fedha hizo walengwa ni kutaka kundi hilo liondokane na umaskini ili nalo liweze kushiriki katika ujenzi wa uchimi wa viwanda kupitia uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo zinatokana na kilimo na ufugaji.

Dkt. Nchimbi alisema kundi hilo halitaweza kupiga hatua kama Watendaji na Waratibu wa TASAF wasipo simama katika nafasi zao na kuwasaidia kuwapa ushauri ambao utawawezesha kutumia fedha wanazopewa katika kujiwekea miradi na hivyo kuondoka katika hali ya umaskini.

“Nyie waratibu na watendaji wengine amuwatendei haki walengwa wa TASAF kama hamusaidia kulima kisasa na kuendesha miradi mimngine kitaalamu…ondokeni maofisi nendeni kwao muangalie wakati wa kulima kama kweli anazingatia kanuni za kilimo bora na kisha muwape ushauri utakaowasaidia” alisema Dkt. Nchimbi.

Alisema watendaji na Waratibu wanapaswa kutembelea mashamba na miradi ya Walengwa wa Mpango wa Kusuru Kaya Masikini kwa ajili ya kuhakikisha kama wanalima pamba au mazao wengi wanalima kitaalamu ili waweze kupata matokeo mazuri ya kilimo chao au ufugaji.

Dkt. Nchimbi alisema kazi ya Waratibu wa TASAF haiishi katika kutoa fedha kwa walengwa pekee bali inakwenda katika kuhakikisha Mlengwa anatumia fedha hizo katika kujilenga maendeleo.

“Mkuu wa Wilaya naomba uhakikishe ninapata taarifa ya watendaji wote na Waratibu wa TASAF wamewatembelea walengwa wamgapi na msaada walitoa kwa walengwa katika kuwawezesha kutumia fedha wanazopata kuboresha miradi yao…waratibu hawapaswi kuiishi katika kuwapa fedha bali ni lazima waennde mbele katika kuwapa ushauri utakao wasaidia kutumia fedha hizo kupiga hatua” alisema Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa.