UBUYU uliopo mezani leo ambao unamung’unywa ni wa chengachenga, lakini ni mlaini na hauchubui ulimi! Ubuyu wenyewe unayeya kuwa, ule ujauzito wa memba wa kundi la muziki wa Bongo Fleva la Scropion Girls, Isabela Mpanda ‘Bella’ unadaiwa ni wa mfanyabiashara ‘pedeshee’ matata wa Bongo, mwenye maskani yake jijini Kampala nchini Uganda, Jack Pemba.

Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ulibaini kuwa, Bella amekuwa akidai kwamba, mwaka mmoja uliopita alikuwa na ukaribu mkubwa na Jack Pemba kiasi ambacho kila mara alikuwa akisafi ri na kukutana na jamaa huyo nchini Uganda. Habari ziliendelea kudadavuliwa kwamba, siyo mara moja, Bella na Jack wamekuwa wakikutana nje ya nchi na mara nyingi mahaba yao walikuwa wakionesha wakiwa huko.

“Yaani Bella na Jack Pemba mapenzi yao walianza kuyaonesha kitambo sana. Kama mtu mwelewa, atagundua wazi walikuwa ni wapenzi, lakini pamoja na hayo, walikuwa wanakutana nje ya nchi mara nyingi sana,” alisema rafi ki mkubwa wa Bella.

Rafi ki huyo alilimwagiwa ubuyu Ijumaa Wikienda kuwa, mahaba hayo ndiyo yalisababisha wakafi kia uamuzi wa kupeana ujauzito ambao kila mmoja aliupokea kwa mikono miwili. Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilianza kuwasaka wahusika hao ambapo lilianza na Bella.

BELLA ANASEMAJE?
Mara baada ya kupatikana hewani, Bella alipoulizwa juu ya ishu hiyo, awali alikataa katakata kutoa ushirikiano. Dakika kumi baadaye, Ijumaa lilipokea simu ya mwanamke mwenye sauti ya mama mtu mzima na kuomba habari hiyo isiandikwe hadi wenyewe watakaapoamua kuweka mambo yao hadharani.

Muda mfupi tena baada ya simu ya mama huyo, Bella alipiga simu na kumuomba mwandishi wetu asiandike chochote hadi kwenye ‘bebi shawa’ yake inayotarajiwa kufanyika Februari 24, mwaka huu ndio kila kitu ataweka wazi.

MIMBA YA WABABA WAWILI?
Hata hivyo, Bella aligoma kutoa namba ya simu ya Jack Pemba ili aulizwe kama kweli ‘mzigo’ huo ni wake kwa sababu kuna ubuyu mwingine unachimbwa unaodai kwamba mimba hiyo ya Bella ina wababa wawili!