Kikosi cha Real Madrid kimeendelea kuimarika katika Ligi Kuu Spain ‘La Liga’ baada ya kuilaza Real Betis ikiwa kwao kwa jumla ya mabao 5-3 na kuifanya sasa kufikisha jumla ya alama 45 ikiwa imecheza michezo 23.

Mabao ya Real Madrid yalitiwa kimiani na Asensio (11′ 59′), Sergio Ramos (50′), Cristiano Ronaldo (65′) na Kareem Benzema (92′).

Real Betis walijipatia mabao yao kupitia Mandi (33′), Nacho (37′) na Sergio Leon (85′).