Msanii wa Hip Hop anayewakilisha Mwanza, Edu Boy amefunguka na kudai amekerwa na kitendo cha Dogo Janja kumuita yeye mtoto mdogo na kumtaka atengue kauli yake hiyo kwani kuoa kwake kusimfanye awe na dharau kwa wengine.

Edu Boy amebainisha hayo baada ya kupita takribani ‘week’ moja tokea Dogo Janja kuzungumza kupitiada ya kupita takribani ‘week’ moja tokea Dogo Janja kuzungumza kupitia eNewz na kudai anamchukulia Edu ni mtoto ambae anahitaji kuisoma vizuri ‘game’ ya muziki ili aweze kukua nayo hivyo hawezi kubishana nae.

“Hii tabia ya Dongo janja ya kuwa anahojiwa kwenye vyombo vya habari aniita mimi mtoto wakati inabidi atengue kauli yake. Kufunga ndoa kusisababishe kuita watu watoto, kuna ndoa nyingine unakuwa unajitwisha mabomu ujue. ‘so’ inabidi awe makini sana, mabomu yasije yakarupuka hadharani akafa na watu”, amesema Edu Boy.

Kwa upande mwingine, Edu Boy amemtaka Dogo Janja awe makini na ndoa yake ili mabomu yakija kurupuka afe mwenyewe.