Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu leo February 19, 2018 ni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH).

Ambapo Rais Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa imesema uteuzi wa Prof. Maboko unaanza leo February 19, 2018.