Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Leo February 19, 2018 amemsimamisha kazi Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Alphonce Sebukoto kutokana na upotevu wa Milioni 279 alizoruhusu zilipwe kwa Mwenyekiti wa Halmashauri kwenye Account yake Binafsi, kwa kazi ya ukandarasi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yupo Mkoani Mwanza katika ziara ya kikazi.