FAMILIA ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline na serikali wamekubaliana kwamba mazishi ya mwanafunzi huyo yatagharimu zaidi ya Sh. milion 60.

Msemaji wa familia, Festo Kavishe, amethibitisha bajeti hiyo kupitishwa na familia na Katibu wa Wizara ya Elimu na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo. Pia Kavishe akisema anayetaka kuchangia msiba huo auwasilishe nyumbani kwa marehemu Mbezi, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo amesema wizara yake ingefanya majadiliano na kuona namna inavyoweza kuchangia gharama hizo.

Pia katika mipango hiyo pamepitishwa ratiba ya mazishi hayo, ikiwemo ratiba ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo Februari 22, 2018 katika viwanja vya chuo cha NIT.

“Mpaka sasa tumekubalina na familia tutaaga mwili wake Alhamisi katika chuo cha NIT saa saba mchana na kusafirishwa nyumbani kwao kwa ajili ya maziko,” amesema Dk. Akwilapo.