Baada ya kuikaba koo Simba katika mchezo wa Ligi uliopita kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga, Mwadui FC imekubali kulala kwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prions leo.

Mchezo huo ambao umepigwa katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, umemalizika kwa bao 1 pekee ambalo limefungwa na nahodha wa timu hiyo, Laurian Mpalile katika dakika ya 54 na kwenda mpaka dakika ya 90.

Huu ni mchezo wa pili sasa Mwadui inapoteza dhidi ya Tanzania Prisons baada ya raundi ya kwanza kufungwa pia mkoani Shinyanga.