MWANADADA machachari kwenye Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ambaye anatarajia kujifungua mwezi ujao, amejikuta akishindwa kufanya shughuli ya maandalizi ya mapokezi ya mwanaye wa kike atakayemzaa ‘baby shower’ kutokana na mambo ya fedha kutokaa kwenye mstari.Habari za ndani zilizonaswa na gazeti hili zilieleza kuwa, awali Gigy hakuwa na mpango wa kufanya shughuli hiyo hadi atakapojifungua, lakini baadhi ya marafiki zake wakamshawishi aifanye Jumamosi iliyopita, lakini siku ilipowadia akagundua bajeti ya shughuli haijatimia.

Alipotafutwa Gigy kuhusu ishu hiyo alisema: “Nilikurupuka kuandaa shughuli ndani ya wiki moja wakati ninataka iendane na hadhi ya jina langu, nikaona isiwe tabu, bora nisogeze mbele hadi wiki ijayo.