Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua mawe yaliyo katwa, Kusagwa na kuongezewa thamani katika kiwanda cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasili katika kiwanda kinachoshughulika na kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Ndg Salim Jesa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kuhusu usafirishaji wa mawe baada ya kuyaongezea thamani wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.


Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua utendaji kazi wa kiwanda cha kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.

Wamiliki wa leseni za madini ya dhababu, vito
na mengineyo kote nchini wametakiwa kuiga mfano wa Ndg Salim Jesa
mmiliki wa kiwanda
cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kinachojishughulisha na kukata, Kusaga na
kuuza mawe kwa kufanya mchakato mzima mpaka bidhaa kukamilika hapa hapa nchini.

Kauli hiyo kwa wamiliki wa leseni za madini
nchini imetolewa leo 20 Februari 2018 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati
akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya.

Alisema kuwa kiu ya serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe
Magufuli ni kuona rasilimali za nchi zinaongezwa thamani zikiwa ndani ya nchi
jambo ambalo linaakisi umakini wa utendaji na ulipaji kodi ya serikali pasina
kukwepa ama kutorosha rasilimali madini yakiwa ghafi.

Aliseama kuwa faida ya kuongeza thamani ya
madini nchini ndio muarobaini wa sekta ya madini kuongeza kiwango cha
uchangiaji wa pato la Taifa hatimaye kufikia asilimia 10% kama ulivyo mpango wa
wizara kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa.

“Nchi nyingi ambazo zimejua siri hii kwa kiasi
kikubwa zimefanikiwa lakini sisi Tanzania tulichelewa sana, na kama
tungeendelea kuchelewa ingefika kipindi ambacho madini yasingekuwepo kamwe na
kama Taifa tungeambulia mashimo makubwa na kusalia katika wimbi la umasikini”
Alisema Mhe Biteko

Aidha, amemuhikishia mmiliki wa kiwanda hicho
kuwa serikali itazungumza na taasisi zinazofanya kazi za ujenzi nchini kuunga
mkono juhudi za umahiri wa kiwanda hicho kwa kununua bidhaa zinazozalishwa
hususani wakati huu ambao serikali inaendelea na mchakato wake wa kuhamia Mjini
Dodoma.

Sambamba na hayo pia uongozi wa kiwanda hicho
umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe
Magufuli kwa kuweka sera nzuri hususani kwa wawekezaji wa ndani katika sekta ya
madini na juhudi zake za kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na serikali kwa
ujumla wake.

Kampuni ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd
iliyopo mkoani Mbeya ilianzishwa mradi wa kukata, kusaga na kuuza mawe Januari
2004 baada ya kukidhi masharti ya usajili wa makampuni