Waziri wa Nishati Mhe. Medadi Kalemani akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyinvua kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Majadiliano wa Miundombinu ya Uchukuzi, Fedha na Afya leo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Speke Resort Munyonyo- Uganda ambao utafuatiwa na Mkutano Kazi kesho wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kushoto ya Mhe. Waziri wa Nishati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda.

Kushoto katika picha ni Mhandisi Joseph Nyamhanga Katibu Mkuu Ujenzi, pembeni yake Prof. Joseph Buchweishaija Naibu Katibu Mkuu Prof. Joseph Buchweishaija, Bi. Amina Kh. Shabaan Naibu Katibu Mkuu, Fedha na Mipango na kulia katika picha ni Mhandisi Shomar O. Shomari Naibu Katibu Mkuu, Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar ni washiriki katika wa Mkutano wa Majadiliano wa Miundombinu ya Uchukuzi, Fedha na Afya unaoendelea kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Speke Resort Munyonyo-Uganda