Msanii Aika kutoka kundi la Navy Kenzo amesema kwa sasa anajihisi mwenye nguvu kiasi kwamba yupo tayari kupata watoto zaidi.

Kauli ya msanii huyo inakuja ikiwa ni miezi miwili imepita tangu ajifungue mtoto wake wa kwanza ambaye amempa jina la Gold. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika anajisikia kuwa ni msichana mdogo zaidi na mwili wake upo huru, yupo tayari kufanya kazi kwa bidii, kutengeneza muziki mzuri, kusafiri dunia na hata kutajaliwa watoto zaidi.

I feel younger, more comfortable in my body, ready to work harder, make more music, travel the world and even make more babies .. Thank you all for ur wishes. Love u all.
December 9 mwaka jana, 2017 ndipo Aika na Nahreel waliweka wazi kuwa wamejaliwa mtoto wa kiume na ilipofika January 12 mwaka huu ndipo waliweka picha za mtoto wao mtandaoni.