Moja kati ya majina makubwa katika soka kutokea ukanda wa Afrika Mashariki basi huwezi kuacha kutaja jina la nadhoa wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta.

Samatta ni moja kati ya mastaa wa soka ambao hawapendi kuweka mali zao hadharani mara kwa mara lakini leo amepost picha ya gari nyeupe lakini kwa mujibu wa maneno yake aliyoyaandika May 26 2015 katika picha ya Range Rover yake aliyoipost instagram, gari ya leo pia inatajwa kuwa ni lake.

“Hello insta friends off to trainning this morning #Vboss hii picha inamaelezo mengi sana ambayo nahisi nikiyaandika apa naweza kuharibu pia, bora nikae kimya lkn nadhan picha yenyewe itatoa somo especially kwa wachezaji uzao wa sasa ktk soka la tanzania.
NB.nshaacha toka 2012 kupiga picha kwny magar ya watu.”
Hivyo baada ya leo kupost picha Mbwana Samatta akiwa katika gari nyeupe, wengi wameatafsiri tu hiyo ni gari yake mpya japokuwa kwenye caption ameweka emoj pekee lakini kwa mujibu wa maneno yake kuwa “Nishaacha toka 2012 kupiga picha kwny magar ya watu” aliyoiandika mwaka 2015 inadhihirisha kuwa gari hilo ni lake, hii ni gari ya tatu Mbwana Samatta kwa gari zake zilizopo Ubelgiji baada ya Mercedes Benz mbili nyekundu na nyeusi alizowahi kuzipost.