Msanii wa muziki nchini Tanzania, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema hawezi kuthubutu kwa sasa kupigana na mume wake Uchebe kwa kwa madai amekuwa na mapenzi ya kupigana yalikuwa ya utoto.
Shilole amebainisha hayo  baada ya kuzoeleka na watu wengi kwa tabia yake ya kupiga wanaume ambao anakuwa nao katika mahusiano na kusema kwa sasa hawezi kuthubutu kufanya hivyo na kama atampiga mume wake basi ni wakiwa faragha nasio pengine.

“Mume wangu ni mwanaume mwenye msimamo katika jambo lake ambalo anataka kulifanya. Siwezi kupigana nae maana alikuwa anapigana kabla ya kuwa nami na ana mkanda huyo usimuone hivyo. Mambo ya kupigana yalikuwa zamani ya kitoto lakini sasa hivi nimekuwa siwezi kusema nataka kupigana na mume wangu wala mume wangu hawezi kusema ainue mkono anipige”, amesema Shilole.

Pamoja na hayo, Shilole ameendelea kwa kusema “mimi ni mtu makini sana ninaejitambua na kujithamini, endeleeni kufuatilia harakati zangu ambazo ninazifanya katika haya maisha.