MWANAMITINDO maarufu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda, ambaye awali alikuwa meneja wa staa mkubwa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, amepata kigugumizi kikubwa cha kuelezea kuhusu mrembo huyo kurejesha penzi lake na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumza na Amani, Kadinda alipata kigugumizi hicho baada ya kuulizwa endapo mastaa hao watarudisha mapenzi atalichukuliaje suala hilo ambapo alishindwa kufafanua badala yake aliishia kuguna na kuomba kama kuna swali lingine aulizwe.

“Jamani mimi siwezi kuzungumza chochote kuhusu hilo na hata sijui nianzie wapi kuzungumza lakini kama kuna ishu nyingine yoyote nitazungumza kwa mapana yote lakini siyo hilo hata kidogo kwa kweli,” alisema Kadinda.
Wema anatajwatajwa kurudisha ‘majeshi’ kwa Diamond baada ya hivi karibuni, mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutangaza kummwaga Diamond.