Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma maneno yalioandikwa kwenye jiwe la msingi mara baada ya kufungua jengo la upasuaji kwenye hospitali ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu kama ishara ya ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima lenye vyumba 43 vya kufanyia kazi.

Makamu wa Rais akimsabahi Mtoto Mchanga pamoja na Mama yake Bi. Mariam Patrik mkazi wa Nyashimba ambaye amejifungua katika wodi ya wazazi ya hospitali ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kufungua jengo la Upasuaji lililopewa jina la Samia Suluhu Hassan Operating Theatre.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Maswa mara baada ya kufungua jengo la upasuaji.

Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais