MSANII anayetamba na Wimbo wa Bajaj, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amejikuta kwenye msongo wa mawazo baada ya mwanamke aliyekuwa mbioni kumuoa aitwaye Iptisam kuolewa na mtu mwingine, kutokana na mvutano wa dini baina yao.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na msanii huyo, Mo Music alikuwa ameshatoa posa hadi mahari lakini tatizo likawa kwenye dini; yeye Mkristo binti Muislam na wote hawakuridhia kutoka kwenye dini zao, ndipo msichana huyo akachumbiwa na mtu wa dini yake na kuamua kumtosa mshkaji bila kurudisha mahari.
Kutokana na ishu hiyo paparazi wetu alimvutia waya Mo Music ambaye alikuwa na haya ya kusema; “Dah umenitonesha kidonda, ni kweli demu kaolewa wiki iliyopita, kitendo cha kubadili dini ningewakera wazazi wangu ndo’maana nikawa nasuasua, tupo kwenye mvutano waturudishie mahari yetu wanatuzungusha.”