Huwezi kuamini! Kikosi cha Simba kimefanywa kama wafalme ndani ya ndege ya Kenya (KQ) kwa kipindi chote cha safari yao.

Iko hivi, baada ya wafanyakazi kujua msafara ule ni wa Simba, kila waipokuwa wakitoa matangazo yao ndani ya ndege walikuwa wakiwatangaza na Simba wakiwapongeza kwa ushindi na kuwatakia mafanikio mema katika mechi zijazo.

“Bila kusahau  ndani ya ndege hii tupo na Wachezaji wa Simba wanaotoka Djibouti na wamefanya vizuri katika mechi yao huko, hivyo sisi wafanyakazi wa ndege hii tunawapongeza sana, tunataka waendelee kufanya vizuri zaidi na zaidi na kuwa wawakilishi wazuri Afrika,” alitangaza mfanyakazi huyo akitumia Lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Simba imewasili usiku wa kuamkia Alhamisi kwa makundi wakitumia ndege ya KQ na. wataingia kambini hii leo Ijumaa.