MUUZA nyago machachari kwenye video za wasanii Bongo, Tunda Sebastian amefunguka kuwa ameufyata mdomo wake kuzungumzia chochote kuhusu aliyekuwa mpenzi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kudai kuwa kila anapozungumzia, Wabongo wanamtusi.

Tunda alisema ameamua kutomzungumzia Zari kwa sababu chochote atakachozungumza watu wataanza kumshushia mvua ya matusi na familia yake haipendi kuona watu wakimporomoshea matusi.


“Mimi kuhusu Zari au sijui ishu za kuachana kwao na Diamond au kitu chochote sitaki kabisa kuzungumzia maana wengine damu zetu ni kama za kunguni nikisema chochote itakuwa shida,” alisema Tunda.