MY AMERICAN EXPERIENCE” picha ya risiti niliyolipia harusi yangu Hotelini Villanova Hotel/New Rochelle nililipia USD 13,000 hahaha nimeikuta maktaba…Miaka 5 ya kuishi na mke na watoto 2 bila kazi ikaanza pole pole to take a toll on me kwa bahati kubwa Mke wangu akapata kazi Ubalozini sasa kikaja kivumbi cha kubadili Status yake ili ifanane na kazi anayoifanya Sheria ya USA ili ubadilishiwe Viza ni lazima utoke nje ya USA ndio urudi so akashauriwa aende Visiwa vya Bermuda siku hiyo nikatoka kazini mapema nikampelekea JFK Airport na mtoto wangu wa Miezi 3 wa kike mimi nikabaki na wa kiume wakaondoka Bermuda so uhakika ulikua watarudi kesho yake na ilipofika kesho yake zikaja Bad News kua walipokua wanarudi Uhamiaji hawakuridhishwa na makaratasi yao..BOOM wakamua kuwarudisha Tanzania kupitia South Africa kwa kizungu inaitwa DEPORTATION kwa Sheria za USA ukishafanyiwa hivyo huruhusiwi kurudi USA tena mpaka baada ya Miaka kuanzia 11 habari hizi zilinikuta nikiwa kwenye gari langu naendesha kurudi nyumbani kutoka kazini nilipigiwa simu na Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania New York Marehemu Simba ndiye aliyenipa the Bad News ilinibidi ni park Gari pembeni furaha yote ya kusubiri mke wangu na mtoto wangu wa kike warudi nikawachukue Airport ikafa hapo hapo na nikaanza kufikiri ninafanya nini na mtoto wangu wa kiume nyumbani bila Mama yake lakini nikashukuru Mungu kua tulikua na House Girl kutoka Tanzania nikaendesha tena mpaka home..katika Maisha yangu nimekua nikipigana sana na Shetani ambaye huwa naamini ni yule yule mmoja anayebadili badili tu mbinu za kunishambulia hapa nikakumbuka kua kanirudia tena maana kwa muda mrefu alikua amenipa break ninaanzia wapi kupigana na hili tatizo jipya na la kutisha? ..nilipofika nyumbani nikamfahamisha House Girl kuhusu yaliyotokea nikamuomba sana awe mstaarabu na mtoto wangu wa kiume yule Msichana akaanza kulia bahati nzuri my son alikua Shuleni ingawa alikua mdogo sana nikamuomba sana House Girl asimuonyeshe kua kuna tatizo amepeleke kucheza as much as inapopatikana tu nafasi ili kumfanya asipate muda wa kumfikiria Mama yake na nikajaribu sana kuhakikisha siri ya hili tatizo haivuji kwa Wabongo I was wrong! ..ITAENDELEA

SHARE
Previous article
Next article