MY AMERICAN EXPERIENCE” kwa mara ya kwanza nilikubali kua Shetani ameniweza ilikua furaha kubwa sana kwa Wabongo mjanja kapatikana sikijua kua kumbe Miaka 5 ya mke wangu kuishi bila kazi na maisha mazuri iliwaumiza sana Wabongo na the worst ilikua kupata kazi nzuri Ubalozini wakati Wabongo wengi wanatunza Wazee na Matahira ilizidi kuwaumiza na sasa wamepata ahueni ya yaliyonikuta ilikua ni furaha hasa kila nilipopita nikikutana na Wabongo ilikua huzuni tupu maana I could tell kicheko cha kishetani usoni mwao…hatimaye nikafanikiwa kuongea na mke wangu nakumbuka kilio chake kwenye simu nilikua nampa moyo kuna atarudi asiwe na wasi wasi miyoni mwangu I felt guilty kwa sababu Wazazi wake walimpeleka Belgium ambako alikua anaishi na sasa nimemuhamishia USA yamemkuta haya so ni tatizo langu zaidi sio lao kwanza nikaanza kwa kumtumia pesa nikaomba kwa mara ya kwanza kuongea na Mama yake mzazi na yeye nikajikaza na kumwambia asiwe na wasi wasi akaniambia jirani ameshamwambia ukweli wote kua hakuna uwezekano kabisa kwa Sheria za USA nikakata simu … my son alikua na tabia ya kusikiliza music mmoja huo huo hata mara 10 bila kuchoka nilikuepo music wake ukawa unapiga sana kelele nikaamua kuuzima ohh my God kwa mara ya kwanza akalipuka “Dad why did you turn off the music? WHERE IS MY MOM?” “WHERE IS MY MOM?” kwa mara ya kwanza machozi yalinitoka mbele yake nikamrudishia music wake akatulia ila ujumbe wake ulikua umefika Loud and Clear …my son alipozaliwa Mama yake aliumwa so kazi ya kumtunza like miezi 3 ya kwanza ilikua yangu mpaka alipo pona nikaanza kumfundisha namna ya kum handle so nilijiamini kua ninamjua sana lakini hii siku alinishangaza kuliko maelezo yaani kumbe anajua kua Mama yake hayupo so kwa mara ya kwanza nikampigia Mama yake na kumpa aongee naye ilisaidia kidogo sana sasa zikaanza marathon za kupigana kumrudisha mama yake zikawa Front 2 kwangu na yeye from Bongo na at the time mke wangu alikua na Mjomba mwenye madaraka makubwa sana Wizara ya Nje lakini alipomfuata Mjomba alimtolea nje maana alishasikia habari nzima akamuambia hayo mambo yatamharibia kazi so mlango mmoja muhimu wa msaada ukawa umefungwa mapema sana! …ITAENDELEA!