MREMBO kutoka Kenya, Vera Sidika hivi karibuni alisema hajawahi kukutana na mwanaume mwenye vigezo vyote ambavyo anavitaka, mazingira yaliyomfanya mpaka leo awe hajawahi kupenda.
Akijibu swali kutoka kwenye mtandao mmoja wa burudani nchini humo juu ya ujumbe aliouandika kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram kwamba, wanaume wengi wanaovutia hawana pesa na wengi wasiovutia ndiyo wana pesa, Vera alisema:

“Ni kweli wanaume wengi ninaokutana nao lazima utakuta wana kitu kimoja, mvuto lakini hawana pesa au pesa lakini hawana mvuto. Sasa kwa upande wangu ninahitaji kumpenda mwanaume mwenye vitu vyote jambo ambalo sijawahi kukutana nalo na ndiyo maana sijawahi kupenda