Msanii wa muziki Bongo, Dayna Nyange amefungua tetesi za kuwa mjamzito.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Komela’ kwa sasa hana ujauzito ila anachokumbuka kwa sasa ni ujauzito wake wa kwanza ambao aliupata akiwa na umri wa chini ya miaka 18.

“Nilipopata ujauzito sikuwa najua, nilikuwanahisi ni Malaria nikaambiwa niende kupima pale hospital ile karatasi ya majibu nilipewa nikambiwa nipeleke nyumbani nilipofika nilimkabidhi dada yangu sikujua kama ni majibu kuwa ni ujauzito,” amesema Dayna.

Dayna ameongeza kuwa mtoto wake kwa sasa ana umri wa miaka 11 na anahitaji afike mbali kielimu asiwe kama yeye ambaye alishindwa kumaliza elimu ya sekondari.
Siku ya wapendanao (Valentine Day) February 14 mwaka huu aliposti picha katika ukurasa wake wa Instagram ambayo ilipelekea wengi kudhani Dayna ni mjamzito.