Msanii kutoka label ya WCB, Queen Darleen ametia neno katika ile drama ya Diamond na Zari The Boss Lady.

Muimbaji huyo ambaye ni ndugu na Diamond ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa kwa mara ya kwanza alishtuka kusikia Zari na Diamond wameachana ila ni kitu ambacho hadi sasa hakiamini.
“Off corse nilishtuka kuona vile nikahisi kama utani na sikutaka kuuliza au kuhoji kwa sababu ingeniumiza ila sitaki kuuliza au kuhoji kitu chochote,” amesema Queen Darleen.


“Kwa imani yangu naona bado wapo wote, kama wameachana, hawajaachana sitaki kujua na ninachojua wapo wote na ninaacha iwe hivyo katika nafsi yangu,” amesisitiza.
Siku ya wapendanao (Valentine’s Day) February 14 mwaka huu Zari The Boss Lady alitangaza rasmi kuachana na Diamond kutokana na kuchoshwa na habari za kusalitiwa ambazo husikika kila siku katika vyombo vya habari.