UHABA wa wafanyakazi ikiwemo kukosekana kwa mwanasheria katika Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Kisiwani Pemba ni miongoni mwa matatizo yanayochangia kokosa ufanisi wa shughuli za Idara hio.

Hayo yameelezwa na Afisa Mkuu Idara ya Maendeleo ya Uvuvi SHARIF MOHAMMED FAKI, katika mkutano wa pamoja na wasaidizi wa sheria katika kuboresha uwezo wa utekelezaji wa usimamizi na sheria na kanuni za uvuvi uliofanyika Wesha, Wilaya ya Chake Chake.

Mkuu huyo alisema kuwa, pamoja na jitihda kuwa zinazofanyika katika kupiga vita na kupambana na wanaopingasheria za matumizi halali ya bahari, bado wanahitaji kuwa na mtu anaeelewa masula ya sheria ili, aweze kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.

‘’Hili linatukwaza sana mikutano tunafanya na wadau mbali mbali kila tunapokuwa na wasaa wa kufanya hivo lakini tumekosa mwanasheria ambae ni maalum kwa ajili ya masuala yetu na ndio maana dhana za uvuvi zinaendelea kutumika visivyohalali’’, alisema Afisa huyo.

Sambamba na hayo, SHARIF aliwasisitiza wadau na wasaidizi wa sheria kuwa kitu kimoja katika kutekeleza majukumu ya kiserikali na kuwaelewesha wanajamii juu ya athari ya uharibifu wa mazingira ambayo ndio tegemezi la taifa.

Kwa upande wake, ABDALLA YAHYA SHAMHUN, kutoka ofisi ya Mrajis Pemba, alieleza kuwa, pamoja na tatizo la wafanyakazi linaloikabili Idara hiyo, ufuataji na usimamizi wa sheria unahitajika wasimimizi wenyewe, ili kuona kanuni zinatekelezeka na kupambana na waharibifu wa mazingira ya bahari kwa faida ya wote.

‘’Tumepata uelewa nzuri pamoja na sisi kusaidia kwetu tunaomba Idara ya maendeleo ya Uvuvi inatakiwa ijikite zaidi katika kusimamia hizi sheria ziweze kutekelezeka ‘’, alisema Afisa huyo.

‘’Ushahidi ndio kitu pekee unaweza kukamata na ukitimiza ushahidi, sisi tutatoa adhabu kwa mujibu wa sheria, ikiwemo faini, kifungo, na mambo mengine yalioelezwa ndani yake, hatutatoka nje ya sheria’’, SHAMHUN alizidi kueleza.

Sambamba na hayo, HASSAN BABU ambae ni Msaidizi Kamanda KMKM Kamandi ya Pemba, alisema kuwa Idara ya uvuvi inajukumu la kujiridhisha katika mitego inayotumika, ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli zao kabla ya kutoa leseni kwa wahusika.

Hata hivyo amewataka wananchi kuacha kutumia mitego haramu ambayo inachangia uharibifu wa mazingira ya bahari hali ambayo inapelekea upotevu wa mazalio ya samaki.

‘’Mafunzo yametuongezea uelewa kwa kiasi tulichopatiwa na tunaahidi kuyafanyia kazi kwa njia zinazokubalika, tunaamini lengo linafikiwa kwa faida ya nchi nzima’’, alisema Afisa huyo.

Mapema katika mkutano huo Afisa mipango kutoka Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Pemba, ALI RASHID HAMAD, tumaini ya Idara hiyo ni kufungua ukurasa mpwa zaidi kwa kutafuta manufaa, ili kuona kwamba wanaokwenda kinyume na sheria wanashughulikiwa ipasavyo.

Mkutano huo ambao ulishirikisha wadau mbali mbali wakiwemo Maafisa wa Idara ya Uvuvi, Idara ya Mahkama, Vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja Jeshi la wanamaji KMKM.