BASI la abiria Kampuni ya Fikoshi Investment linayofanya safari zake kati ya Kaisho, Bukoba na jijini Mwanza limepata ajali katika eneo la Nkwenda Wilayani Kyerwa mkoani Kagera na kusababisha kifo cha kondakta wa basi hilo.


Kondakta wa basi hilo ambaye bado hajafahamika jina lake, alifariki papo hapo, huku majeruhi kadhaa wamekimbizwa katika Hospitali teule ya Nyakahanga na wengine katika Kituo cha Afya Nkwenda kilicho karibu na eneo la ajali.