MARA baada ya kuokoka, mtangazaji Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ ameamua kugeukia Muziki wa Injili ambapo ameanza kufanya mazoezi ya kuimba.

Aunt Lulu alisema kuwa ameamua kumuimbia Mungu hivyo yupo mazoezini na hivi karibuni watu wakae mkao wa kula kwani ataimba wimbo wenye kuelimisha jamii.

“Natarajia kuimba vitu vya ukweli ambavyo vinaihusu jamii, iwapo mtu atasikiliza atapata elimu hivyo mashabiki wa nyimbo za Injili na mimi wanisubiri nitatoa kitu cha maana yaani watu hawataamini,” alisema Aunt Lulu.