Country Boy ambaye wimbo wake wa Turn Up unafanya vizuri kwenye gemu la Muziki Bongo Fleva, hivi karibuni alifunguka kwamba ikiwa atapata nafasi ya kufanya kolabo kwa sasa mtu pekee anayemfikiria ni mwanamama Khadija Kopa.

Akipiga stori na Showbiz, Country alisema Khadija Kopa ni mwanamuziki mkongwe anayeujua muziki vizuri na kwa upande wake anamzimia sana na siku moja atafanya juu chini ili waweze kupiga kolabo.

“Kiukweli ninamzimia sana Khadija Kopa. Ni mwanamama ambaye anajua muziki na mimi kufanya naye kazi inaweza kunifungulia ukurasa mwingine wa muziki wangu kwa upande wa mashabiki,” alisema Country Boy.