Wakati style ya kubadili rangi ya nywele zao na kuweka rangi tofauti tofauti ikiendelea ku-trend, Mwana FA hajakaa kimya katika hilo.

Katika moja ya picha za Ommy Dimpoz ambazo anaonekana na akiwa amepaka rangi kichwani ambazo ameposti katika Instagram, Mwana FA ameandika; Hivi hizi nywele mmepatwa na nini safari hii nyi watoto kina Defao?smh.
Baada ya kuona comment hiyo Ommy Dimpoz alimjibu Mwana FA; mkubwa ukitaka kutisha piga pink .
Siku za hivi karibuni wasanii wengi wamekuwa wakipaka rangi tofauti tofauti katika nywele zao, miongoni mwao ni Ben Pol, Alikiba, Ommy Dimpoz, Lava Lava, Vanessa Mdee. Hapo awali kulikuwa na Harmonize, Queen Darleen na Amber Lulu ambao wanaendelea hadi sasa.