Mlinda lango wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Aishi Manula amesema kuwa michezo yao miwili hatua ya awali kwenye Kombe la Shirikisho dhidi ya Gendarmerie haikuwa migumu sana ukilinganisha na ubora wa kikosi chao ila kazi ipo pale itakapo kutana na Al Masry.
“Hazikuwa mechi ngumu sana kulinganisha na ubora tulionao kikosi cha Simba chini ya benchi letu la ufundi,” amesema Manula
“Ili kuwa ni michezo ya kwaida sana ila nadhani sasa kwenye mchezo unaofuata ndio tunaanza mashindano rasmi na tunajiandaa vyema sana kwa ajili ya mchezo ule dhidi ya Al Masry ambapo tutaanza nyumbani.”
Simba SC imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 5 – 0 dhidi ya Gendarmerie.
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limethibitisha luwa mchezo huo utapigwa siku ya Jumanne ya tarehe sita ya mwezi ujao na marudiano yake ni siku ya Ijuma ya tarehe 16 huo wa tatu.