Producer ambaye kila siku anatoa hits hapa Bongo, Mr. T Touch amesema yale aliyofanikisha katika muziki ni machache ukilinganisha na kile alichodhamiria.
Mr. T amesema iwapo hadi sasa kama muziki umeshampatia faida anayostahili hawezi kuwa na takwimu za moja kwa moja ila kuna kitu ambacho bado anakihitaji.

“Mimi naona nimetimiza ndoto zangu kwa asilimia ndogo kwa sababu vitu ambavyo naviwaza kuvitimiza ndani ya muziki naona ni vikubwa zaidi kwa hiyo nahitaji kukaza zaidi,” Mr. T ameiambia Clouds Fm.

Ameongeza kuwa huwa hapendi kukata tamaa kwenye kitu ambacho anakifanya na pili anapenda sana kitu ambacho anakifanya na ndio sababu kila siku anajitahidi kupata nafasi ambayo hakuwahi kuwa nayo hapo awali.