Rapa Nay wa Mitego mwenye ‘hit song’ ya ‘Mikono Juu’ amefunguka na kujitetea kwamba kuhusiana na kukatika viuno katika video yake wimbo mpya na kudai ameamua kufanya hivyo ili kujaribu kuonesha umma kuwa naye anaweza jambo hilo.
Nay ameeleza hayo baada ya kupokea ‘comment’ nyingi pamoja na ujumbe mfupi kutoka kwa wadau zake kumshangaa kwa namna alivyokatika kiuno katika video ya wimbo wake mpya huku wengine wakisema alichokifanya sio maadili ya wasanii wa kufofoka (Hip Hop).

“Mimi ndio nilimwambai Nic Class ‘shout’ napiga uno kidogo, lazima ufanye kitu ambacho watu hawakutarajia kukuona fulani atafanya ili mradi ilite utofauti na ndio maana leo tunazungumzia kuhusu vile viuno vyangu katika ‘video'”, amesema Nay wa Mitego.

Pamoja na hayo, Nay ameendelea kwa kusema “wengine huwa tunafanyaga chumbani lakini safari hii tumeamua kuvileta kidogo huku angalau watu wajua kwamba sio hatuwezi, tunaweza. Kujaribu na kufanya utofauti kidogo inaruhusiwa”.